Kuhusu ICR

Assalamu Alaikum Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh

Islamic Centre For Research (ICR) ni kituo kilichoanzishwa mwezi Juni, 2010. Lengo kuu la kituo hiki ni kuhamasisha maarifa ya kidini katika maisha yetu ya kila siku na kutoa huduma za kijamii.

Utafiti unaofanywa na kituo hiki unahusisha mambo yote ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, kielimu n.k kwa maslahi ya jamii ya wanadamu wote.

Msukumo wa shughuliza ICR unatokana na kauli ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur'an Tukufu:
Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.
Qur'an Surat Yusuf 12: 108
 

Miongoni mwa huduma za kijamii ni pamoja na:

1. Elimu
2. Uchapishaji
3.Misaada ya kibinaadamu.
Katika mtandao huu utakutana na tafiti mbalimbali za kitaalamu zinazoendeshwa na kituo sanjali na shughuli nyingine za kituo.

No comments:

Post a Comment