Tuesday, August 21, 2012

KUMBUKUMBU YA 43 YA KUCHOMWA KWA MSIKITI WA AL-AQSA



Siku ya leo ya Jumanne inasadifiana na kumbukumbu ya 43 ya msiba mkubwa uliowakumba Waislamu kwa kuchomwa msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, qiblah cha kwanza cha Waislamu na mmoja wa Misikiti mitatu mtukufu zaidi kwa Waislamu. Katika siku kama ya leo, Waislamu hukumbuka jinai mbaya iliyofanywa dhidi ya Msikiti huo Mtukufu na moto uliowashwa na mikono ya chuki na uadui.

Jinai hii iliamsha moto wa upinzani na hasira kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Siku ya pili baada ya tukio hilo, maelfu ya Waislamu waliswali swala ya Ijumaa katika viwanja vya nje vya Msikiti huo Mtukufu, na baada ya hapo maandamano yakaenea mji mzima wa Qudsi kupinga kitendo hicho, jambo lililopelekea kufanyika mkutano wa kwanza wa nchi za Kiislamu mjini Rabat, Morocco.

 Aidha, tukio hilo ovu lilizusha radiamali (reaction) za kiulimwengu na kimataifa zikilipinga kwa nguvu. Hiyo ikapelekea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa azimio lake namba 271, ambalo liliwatia hatiani wavamizi kwa kuuvunjia heshima msikiti huo na kuzitaka mamlaka vamizi za Israel kufuta hatua zote zitakazoathiri hali ya Mji huo Mtakatifu.

Azimio hilo lilielezea masikitiko ya Baraza hilo juu ya uharibifu uliosababishwa na moto huo kwenye Msikiti chini ya uvamizi wa Israel na kuitaka iheshimu mkataba wa Geneva na sheria ya kimataifa inayosimamia uvamizi wa kijeshi, na kuacha kukwamisha kazi ya Baraza la Kiislamu unaolenga kulinda, kuratibu na kuboresha maeneo Matakatifu ya Kiislamu.

Maadhimisho ya mwaka huu ya kuchomwa kwa msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa yanakuja huku vita kali ikipamba moto dhidi ya Mji wa Qudsi (Jerusalem) kwa ujumla, na hasa msikiti wa Al-Aqsa, baada ya wazo hatari la Israel linalopendekeza kuigawa Al-Aqsa katika sehemu mbili za Waislamu na Wayahudi, pendekezo ambalo litakuwa na athari na matokeo mabaya sana kwa mustakbali wa Msikiti huo.

Vilevile, kumbukumbu za mwaka huu zinaweka mkazo kuwa mji wa Qudsi (Jerusalem) na maeneo yake matakatifu vitabaki kuwa mali ya Waislamu kwa namna yoyote ile, hata kama Utawala vamizi wa Israel utafanya nini katika kujaribu kubadilisha alama za mji huo Mtukufu na kujenga maelfu ya makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika mji huo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisisitiza katika azimio lake lililotoka katika mwezi wa Juni, mwaka 1980 kwamba kuzikalia kwa mabavu ardhi hizo ni jambo lisilokubalika, huku Baraza hilo likisisitiza upinzani wake dhidi ya matendo ya kiuadui yanayofanywa na walowezi katika mji huo. Mwaka huohuo, Baraza lilizitaka nchi zenye balozi katika mji huo kuzihamisha.

Katika azimio la mwezi Juni, mwaka 1998, kwa mara ya kwanza, wanachama wote wa Baraza walikubaliana kuuzuia Utawala wa Kizayuni kujitanua katika mji huo na kuonesha kuwa kufanya hivyo ni kukiuka maazimio ya sheria za kimataifa.

Saturday, August 18, 2012

EID MUBAARAK



Islamic Centre for Research (ICR) inawatakia Waislamu wote sikukuu njema ya Eidul-fitr...
Allah aitakali swaumu zetu na amali zetu tulizozifanya katika mwezi huu adhimu wa Ramadhan!
Amiin!

 

Friday, August 17, 2012

KUMALIZIKA KWA MKUTANO WA JUMUIA YA USHIRIKIANO WA KIISLAMU (OIC) MJINI MAKKAH



Kilele cha mkutano wa dharura wa Jumuia ya Ushrikiano wa Kiislamu (OIC) kimefikia tamati yake mjini Makka kwa kusisitiza juu ya kulinda umoja wa Waislamu na kusimama imara dhidi ya “fitna” katika nchi za Kiislamu. Pamoja na hayo, mkutano huo ulikuwa na maazimio yafuatayo:
1.       Mkutano mkuu umetaka kusimamishwa haraka matumizi ya nguvu nchini siria pamoja na kulipeleka mbele ya umoja wa Mataifa suala la Waislamu wachache wa BURMA (MYANMAR) wanaonyanyasika na kukandamizwa.

2.       Wamelipokea na kulikubali pendekezo la mfalme Abdullah ibn Abdulaziz wa Saudi Arabia la kuanzisha kituo maalumu kwa ajili ya mazungumzo na maelewano baina ya Madhehebu za Kiislamu, kitakachokuwa na makao makuu mjini Riayadh, Saudia.

3.       Viongozi wa  nchi za Jumuia hiyo yenye wanachama 57 ambao wanawakilisha zaidi ya watu bilioni 1.5 duniani,  wamekubaliana juu ya “umuhimu na ulazima wa kulinda umoja wa nchi ya Syria na ardhi zake na kusimamisha mara moja matumizi yote ya nguvu pamoja na kusitisha uanachama wa Syria katika Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu.”

4.       “Azimio la Makkah” limetaka “baadhi yetu kujitenga dhidi ya kutumia misimamo ya kimakundi na kimadhehebu katika kutumikia siasa na malengo yake badala ya kutumia siasa kwa ajili ya kuitumikia dini.”

5.       Tamko la azimio hilo limesisitiza “kusimama safu moja pamoja na jamii za Kiislamu zinazonyanyaswa na kuonewa mbele ya macho na masikio ya walimwengu wote na kukabiliana  na uadui wa kutisha unaofanywa dhidi ya wananchi wasiokuwa na msaada, wanaouawa na kuteswa.”

6.       Vilevile azimio hilo limesisitiza juu ya kusonga mbele katika “mapambano dhidi ya ugaidi na fikra potofu zinazosababisha suala hilo, kuulinda umma dhidi ya hilo janga na kutoyaruhusu makundi yanayochafua historia ya umma huu pamoja na kitabu chake na sunna za Mtume Wake.”

7.       “Kusimama safu moja katika kupambana na fitna ambazo zimeanza kupenya ndani ya kiwiliwili     cha Uislamu kwa misingi ya ubaguzi, madhehebu na makundi. Suala hilo litawezekana kwa kuheshimu utukufu na uhuru wetu na kutoingilia masuala ya ndani kwa kigezo cha nchi moja kuisimamia nchi nyingine na kwa kisingizio cha aina yoyote ile.”

8.       Vile vile azimio limetoa jukumu zito kwa vyombo vya habari katika “kuondosha fitna na kuimarisha misingi na malengo ya ushirikiano na mshikamano wa Kiislamu.”

9.       Pamoja na hayo, viongozi hao wa nchi za Kiislamu walitilia mkazo juu ya “umuhimu wa kadhia ya Palestina kwa kuizingatia kadhia hiyo kuwa ni mhimili wa umma wa Kiislamu na kukomesha ukaliaji wa mabavu wa Israel kwenye ardhi za Waarabu na Palestina tangu mwaka 1967 ikiwemo msikiti mtukufu wa Quds. Waliubebesha utawala vamizi wa Israel lawama ya kukwama kwa mazungumzo ya pande husika.

10.   Kwa upande mwingine, viongozi hao wa nchi za Kiislamu wameazimia kulipeleka suala la Waislamu wa Burma mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, huku wakikosoa vikali matumizi ya nguvu yaliyofanywa na watawala dhidi ya Waislamu hao.
Katika azimio la mwisho la Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu, viongozi hao walielezea “masikitiko yao makubwa kwa utawala wa Myanmar (Burma) kutumia nguvu dhidi yao na kuwanyima haki ya uraia.”

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu, Ekmeliddin Ihsanoglu  katika mkutano wake na waandaishi wa habari baada ya kikao cha mwisho cha Mkutano huo, alisisitiza kuwa viongozi wote wa Jumuia, katika mazungumzo yao, walijikita sana katika kadhia ya Waislamu wa Myanmar (Burma),  jambo linaloisisitizia Jumuia ya Kimataifa na Serikali ya Burma kwamba “zaidi ya Waislamu bilioni moja na nusu wamesimama nyuma ya Waislamu wa Burma.”

Mkutano huo ulikosoa vikali kile ulichokiita “uhalifu wa kibinaadamu” unaofanywa na Serikali ya Myanmar dhidi ya Waslamu wa chache wa nchi hiyo.
“Azimio la Makka” lilisisitiza kuwa “siasa za manyanyaso na matumizi ya nguvu zinazofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya raia wake Waislamu ni uhalifu dhidi ya ubinaadamu na ni jambo linalotakiwa kukosolewa na kupingwa vikali na mataifa yote ya ulimwengu wa Kiislamu kwa namna ya kipekee na mataifa ya ulimwengu mzima kwa ujumla.”
Viongozi hao wa nchi za Kiislamu wameitaka “Serikali ya Myanmar kuacha haraka vitendo hivyo na kuwapa Warohingya haki zao kama raia katika nchi ya Myanmar.”
Mkutano huo ulioitishwa na mfalme wa Saudi Arabia, ulihudhuriwa na marais wa nchi wapatao 40. 

Wednesday, August 15, 2012

MKUTANO WA OIC KUFIKIA KILELE CHAKE LEO MJINI MAKKAH

Viongozi wa Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu katika mkutano wa Jumuia hiyo mjini Makkah, Saudi Arabia
Mkutano wa dharura wa Jumuia ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) utafikia kilele chake leo Jumatano katika mji Mtukufu wa Makkah.

Katika mkutano huo, yatajidiliwa masuala kadhaa ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Mgogoro wa Syria.

Katika kikao cha ufunguzi, mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah Bin Abdul Aziz alitoa wito wa kuanzishwa kwa kituo maalumu kwa ajili ya mazungumzo kati ya madhahebu za Waislamu ambacho kitakuwa na makao yake mjini Riyadh. Mfalme Abdullah pia alipendekeza kuteua wajumbe wa kituo hicho kutoka katika mkutano wa kilele.
Mkutano huo utaangazia masuala kadhaa hasa mgogoro wa Syria, ambao katika mkutano wa maandalizi uliofanyika Jumatatu alipendekeza kusimamisha uanachama wa Syria katika Jumuia hiyo.

Hotuba mbili zilitolewa katika ufunguzi. Ya kwanza ilitolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Ekmeleddin Ihsanoglu, ambaye alisisitiza kuhusu haja ya kuulinda umoja wa Kiislamu, akiashria kuwa kwa sasa ulimwengu wa Kiislamu katika hali ngumu na kwamba anasubiri maazimio muhimu ya mkutano huo.

Mzungumzaji wa pili alikuwa rais wa Senegal Macky Sall, akibainisha uzito wa hatua ya sasa na kusisitiza haja ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Saturday, March 24, 2012

Translators Wanahitajika

Bismi Allāhi Ar-Raĥmāni Ar-Raĥīmi
Assalamu Alaikum Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh
Islamic Centre for Research
(Kituo Cha Utafiti Cha Kiislam Tanzania)

Tunatangaza kuwa, Tunatafuta watu wenye uwezo wa Kutafasiri (Translation) Vitabu Mbalimbali Kutoka Lugha ya Kiingereza au Kiarabu Kwenda Lugha ya Kiswahili.

Vitabu Vinavyotakiwa Kutafasiriwa ni Vitabu vya Dini ya Kiislamu (Spiritual Books)

Sifa za Mwombaji: 
  • Awe Muislam Mwenye Akili Timamu
  • Uwezo wa Kutafsiri
  • Awe amewahi kufanyakazi ya Kutafasiri Nyaraka zenye maudhui ya kidini (Kiislam) kwenye lugha ya Kiingereza au Kiarabu.
  • Awe Mwepesi katika kuifanya kazi bila ya usimamizi!
Tafadhali kama unazo sifa hizo usisite. 
Wasiliana Nasi Kwa Simu Namba:
+255 712 566 595
+255 763 348 213
E-mail:utafititz@gmail.com

Friday, March 23, 2012

Tangazo la Mashindano ya Kimataifa

Al Azhar Al Sharif
Mkusaanyiko wa Tafitit za Kiislamu
Idara kuu ya Mambo ya Baraza la Mkusanyiko na Kamati zake.

(Uwezo wa Kuran Tukufu na Sunnah za Mtume S.A.W. zilizotakasika juu ya mwenendo wa Elimu ya Mazingira)

 Kamati ya Uwezo wa elimu ya Kuran na Sunnah za Mtume Mtakasifu ya Azhar Asharif kwa kushirikiana na Bank Faisal ya Kiislamu tawi la Egypt, inawatangazia kuwa itaandaa Mashindano ya Kimataifa juu ya (“Uwezo wa Kuran Tukufu na Sunnah za Mtume S.A.W zilizotakasika juu ya mwenendo wa Elimu ya Mazingira

Kwa masharti yafuatayo:-
  • Mosi: - Utafiti uandikwe kati ya lugha mbili: - Kiarabu au Kiingereza.
  • Pili: - Utafiti utakaoletwa kwa mshindano usiwe kwa kiwango cha kielimu au umepewa zawadi nyingine.
  • Tatu: - Utafiti uweke wazi juu ya uhakika wa kielimu ambao umetanguliwa na Kuran pamoja na Sunnah Takasifu.
  • Nne: - Utafiti uandikwe kwa Kompyuta na usipungue kurasa mia moja na zisizidi kurasa mia mbili, pamoja na Ufupisho ulio nje ya Utafiti usiopungua kurasa kumi na usiozidi kurasa ishirini pamoja na CD inayohusu utafiti huo.
  • Tano:- Utafiti pamoja na Ufupisho wake upelekwe na taarifa binafsi ya mashirika (C.V.) kwa nakala tatu kwenye Kamati ya Uwezo wa Kuran Tukufu na Sunnah za Mtume – Mkusanyiko wa Tafiti za Kiislamu Nasr City mpaka mwisho wa mwezi Mei 2012 na mpelekaji wa utafiti huo atapewa risiti iliyogongwa.
  • Sita: - Baada ya kupitiwa kwa tafiti na wahusika washindanaji wataitwa wenyewe kwa wale waliopendekezwa kufuzu na kupewa zawadi za mali kwa kiwango cha:- 

Paundi Elfu Hamsini na Tano za Kimisri (55,000/=) kwa washindani ishirini na tatu (23) kama ifuatavyo:- Paundi 15,000 elfu kumi na tano kwa mshindi wa kwanza.  Paundi 10,000 elfu kumi kwa mshindi wa pili. Paundi 5,000 elfu tano kwa ,mshindi wa tatu.

Na zawadi tano (5) za kutia moyo zitatolewa kwa watu watano ikiwa kila mmoja atapata Paundi Elfu mbili (2,000/=)

Na zawadi kumi na tano (15) nyingine za kutia moyo zitatolewa kwa watu watano ikiwa kila mmoja atapata Paundi Elfu moja (1,000/=)

  • Saba: - Watapewa taarifa washiriki wa shindano sehemu na siku ya sherehe ya kuzawadia washindi.
  • Nane: - Tafiti iliyoshinda haitarejeshwa kwa mwenyewe, kwani tafiti hiyo itahifadhiwa kwenye ofisi za Kamati maalum kwenye jingo la ofisi za Azhar Asharif, ama kwa tafiti zisizoshinda zitarudishwa kwa wenyewe kwa kipindi cha miezi miwili tokea tarehe ya sherehe ya kugawa zawadi.
  • Tisa: - Kwa mwenye kutaka kujifanyia waqfu achapishe na kusambaza yale atakayopata toka kwemye tafiti ya mshindi, kwa gharama ya waqfu bila idhini na haki toka kwa mshindi.
  • Kumi:-Tangazo hili linahusu Vyuo vVkuu vyote na Vituo vya eEimu pamoja na Magazeti na wasambazaji – kama habari isiyo na malipo – kwa Magazeti na Majarida mbalimbali.

Mwenyezi Mungu ndiye Mwezeshaji wa kila jambo.

Kamati ya uwezo wa Elimu ya Kuran Tukufu na Sunnah za Mtume zilizotakaswa Mkusanyiko wa Tafiti za Kiislamu

Ugonjwa Wa Kichocho (Bilharzia)

Tatizo hili huwapata watu wengi hasa watoto wanaocheza katika madimbwi ya maji wakati wa mvua au wanapotumia maji ambayo yana vijidudu vya maradhi hayo. Vijidudu vya kichocho humuingia binadamu na kwenda kuishi katika kibofu cha mkojo au utumbo wake.

Kwa kawaida kimelea cha kike hutaga mayai ambayo hutoka kwa mtu mwenye ugonjwa huo na kuingia katika maji ikiwa mtu huyo atakojolea maji hayo au wakati wa haja kubwa. Mayai hayo huanguliwa na kutoa viluilui ambavyo hupenya kwa konokono wa majini. Viluilui hawa baada kutoka kwenye mwili wa konokono huweza kumuingia binadamu na kupenya katika ngozi na kwenda kutulia ktka mishipa ya ini ambapo hukomaa na baada ya hapo hutoka na kuingia katika mishipa ya kibofu cha mkojo na njia ya haja kubwa  katika utumbo mpana.

Mgonjwa asipotibiwa haraka hupata matatizo katika njia ya haja kubwa na kibofu cha mkojo na wakati mwingine mayai ya kichocho huingia katika uti wa mgongo au katika ubongo na kusababisha matatizo.

Dalili
Kupatwa na homa siku 30 baada ya kunywa maji yenye maambukizi
Kikohozi kikavu na kujihisi kuchoka.
Baadaye damu huanza kutoka kwenye mkojo na haja kubwa lakini hatua hii ni baada ya ugonjwa kukomaa.

Ushauri
Kichocho ni ugonjwa unaotibika haraka kwa dawa iwapo itabainika mapema.
Watoto wazuiwe kuogelea katika madimbwi au maji yaliyosimama.
Kunywa maji masafi na salama.
Wanaoish kando ya mito, maziwa na bahari wasikanyage maji hayo bila kuwa na viatu maalumu vya kuzuia maji kupenya na mabwawa yote ya kuogelea yawekwe dawa ya kuua vijidudu.

Makala Haya Yameandaliwa Na Dokta Abdulazizi Maliki
Simu:
+255 714 909 563
+255 763 986 499